Alhamisi, Machi 31, 2016

VIPI KUHUSU SARATANI YA MATITI KWA WANAUME??

Ingawa kuna matukio machache sana, lakini kuna wanaume wanaopata saratani ya matiti. Chuo kikuu cha Leeds kimetoa ripoti ikisema, wanaume wakinenepa zaidi, hatari ya kupata saratani ya matiti itaongezeka zaidi.
Sawa na wanawake, wanaume pia wanakibiliwa na hatari ya kupata saratani ya matiti. Kimeng’enya kilichoko ndani ya celi za mafuta za wanaume kinaweza kubadilisha homoni ya kiume kuwa homoni ya kike. Mafuta yakiongezeka mwilini mwa wanaume, homoni nyingi zaidi za kiume zinaweza kubadilishwa kuwa homoni za kike.
Watafiti wa chuo hicho wamegundua kuwa asilimia 90 ya seli za saratani ya matiti ya wanaume zinaweza kutambua homoni za kike, na kuanza kuenea mwilini. Hicho ndicho chanzo cha wanaume wanene kuweza kupata saratani ya matiti.
Mbali na hayo, lehemu (cholesterol) inaweza kubadilika kuwa kitu kimoja ambacho kina kazi sawa ya homoni ya kike. Kiwango cha lehemu cha wanaume wanene ni cha juu sana, hivyo hatari ya saratani ya matiti pia itaongezeka.

0 comments:

Chapisha Maoni