Alhamisi, Machi 31, 2016

MACHUNGWA NI KINGA BORA YA MAGONJWA

Utafiti wa Japani umeonesha kuwa afya inaweza kunufaika kutokana na kula machungwa kila siku, wanaokula machungwa mara kwa mara wanakabiliwa na hatari ndogo kupata ugonjwa wa kisukari wa aina II na maini yenye mafuta. 
Tasisi ya tekonolojia ya kilimo na chakula ya Japani na chuo kikuu cha matibabu cha Hamamatsu zimesema, watafiti wao walifanya utafiti uliodumu miaka 10, ambao uliwashirikisha watu elfu 1. Moja kati ya malengo ya utafiti huo ni kutafiti uhusiano kati ya afya na tabia ya kula machungwa.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, kwa kulinganishwa na watu wasiokula machungwa, hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari wa aina II kwa watu wanaokula machungwa 3 au 4 kila siku inapungua kwa asilimia 57. 
Watafiti wanaona kuwa cryptoxanthin iliyomo ndani ya machungwa ni chanzo kikuu cha kinga ya maradhi hayo. Cryptoxanthin pia ina kazi ya kuhakikisha afya ya mifupa na kukinga saratani.

0 comments:

Chapisha Maoni