Polisi wameimarisha usalama kisiwani Zanzibar kabla ya duru ya pili ya uchaguzi kesho Jumapili.
Kamanda wa polisi Mkadam Khamis Mkadam amesema watahakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa amani.
Chama cha Upinzani CUF kimesema kitasusia uchaguzi huo huku chama tawala CCM kikisisitiza kuwa kitashiriki.
CUF kinasema mgombea wake wa urais Seif Shariff Hamad alishinda kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Matokeo ya uchaguzi wa kwanza yalifutiliwa mbali na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa sababu za “ukiukaji mkubwa wa taratibu.”

0 comments:
Chapisha Maoni