Jumatatu, Machi 21, 2016

TISHIO GANI LINAUKABILI ULIMWENGU?

Ulipotimia mwaka mmoja tangu ajali ya kuanguka kwa ndege ya Germanwings, mwandishi wa Uingereza Bw. Simon Kuper aliandika makala kwenye gazeti la “Financial Times” akizungumzia sababu za kibinadamu kuwa tishio kubwa zaidi linaloikumba dunia kwa sasa. Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Kuper, mauaji, mapambano, ajali za ndege, na mashambulizi ya kundi la IS, ni hatari zaidi kwa usalama wa binadamu kuliko magonjwa makubwa. Mwaka 2014 kwa mfano idadi ya watu waliouawa kwa kupigiwa risasi nchini Marekani ilikuwa sawa na idadi ya watu waliofariki kwenye ajali za barabarani kwa mara ya kwanza katika miaka 60 iliyopita. Lakini Bw. Kuper ameongeza kuwa baada ya miongo kadhaa, matishio makubwa zaidi kwa binadamu yatakuwa roboti zisizodhibitwa na binadamu, na hali ya hewa. 
Wewe unaona ni tishio gani linaikumba zaidi dunia kwa sasa, na kwanini?

0 comments:

Chapisha Maoni