Jumanne, Machi 22, 2016

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUPATA MAFUNZO YA BUNGE KUTOKA CHINA, NCHI NYINGINE ZA AFRIKA NA ASIA KUNUFAIKA

Serikali ya China itazindua mradi maalum wa kutoa mafunzo kwa wabunge kutoka nchi za Afrika na Asia ikiwa ni mojawapo ya njia za kuboresha huduma za bunge kwa wananchi wa nchi zinazoendelea, Zhang Dejiang, afisa wa ngazi za juu katika bunge la China amesema.
Bw. Zhang alitangaza rasmi mpango huo akiwa nchini Zambia katika mkutano wa kiamsha kinywa na viongozi wa bunge kutoka Zambia, Rwanda, Kenya, Pakistan, Bangladesh na Cambodia. Akihutubuia kongamano la wabunge mjini Lusaka, Zhang alisema kuwa Uchina, ambayo inaorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayoendelea, itasimama imara na nchi zinazoendelea kulinda maslahi yao.
Kiongozi huyo wa chama cha kikomunisti alisema kuwa Uchina imefanikiwa kuendeleza siasa zake kupitia mfumo wa ujamaa ambao unaambatana na itikadi zake, huku akiongeza kuwa demokrasia inaweza patikana kupitia mifumo mbali mbali.
Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa bunge la China kuhutubia kongamano hilo. Ziara ya Zhang katika bara la Afrika ilianza Mechi 18 na itaendelea kwa siku kumi hadi Mechi 27. Kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea Rwanda na Kenya katika ziara hiyo muhimu.

0 comments:

Chapisha Maoni