Jumatatu, Machi 28, 2016

MWANAMKE WA MIAKA 68 AMUUA KWA KISU MUMEWE KWA KUMALIZA CHAKULA JIKONI

Mwanamke mmoja wa miaka 68 anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi cha Kakamega nchini Kenya kwa tuhuma za kumchoma mme wake mwenye miaka 79 kwa kisu mpaka akafariki.
Majirani wa familia hiyo wanasema tukio hilo lilitokea baada ya marehemu kula chakula chote kilichokuwa kimeachwa kwenye sufuria.
Mtuhumiwa alishikwa na hasira na kumshambukia mme wake kwa kisu cha jikoni.

0 comments:

Chapisha Maoni