Jumatatu, Machi 28, 2016

MATOKEO YOTE YA MECHII ZA CHAD KUNDI G YAMEFUTWA BAADA YA KUSHINDWA KUFIKA TANZANIA, TAIFA STARS KUBAKI MKIANI

Timu ya Taifa ya Chad imejitoa kwenye mashindano yanayoendelea ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, 'Afcon 2017' wakitoa sababu ya ukata wa fedha kuelekea mechi yao ya pili dhidi ya Tanzania ambayo ilipangwa kufanyika Machi 28 uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo ya Afrika ya kati ilipoteza dhidi ya Taifa Stars Jumatano ambapo Tanzania iliandika ushindi wa kwanza kwenye michuano hio mikubwa zaidi barani Afrika.
Barua iliyoandikwa na mamlaka ya michezo Chad imesomeka "Kama sehemu ya ushiriki wetu kwenye michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon 2017 na hasa mechi yetu ya marudiano na Tanzania, tunatoa angalizo kwamba timu yetu ya taifa imeshindwa kufika kwenye mechi ya marudiano Dar es Salaam Machi 28"
"Tunawatakia kila lakheri na tunaomba radhi kwa hali hii" Ilisomeka sehemu ya barua hio. Chad wanashikilia mkia kwenye kundi G bila alama yoyote baada ya kufungwa mechi tatu.
Kulingana na kanuni za shirikisho la michezo Afrika(CAF) matokeo yataondolewa hivyo mechi za Chad kwenye kundi G hazitahesabika, hio inamuacha Misri kubaki kinara wa kundi na alama nne, akifatiwa na Nijeria mwenye alama 2 na Tanzania kubaki na alama moja, Misri na Nijeria mechi yao itajechezwa Machi 29 mjini Alexandria. Pia kundi kundi G halitaweza tena kutoa mshindwa bora 'Best looser' kwani makundi yenye timu tatu huwa hayatoi mshindwa bora hivyo timu pekee itakayoenda Afcon nchini Gabon ni ile itayokuwa kinara wa kundi pekee.

0 comments:

Chapisha Maoni