Watafiti wa Australia wamegundua kuwa kama panya wa jaribio wakifanya mazoezi katika kipindi cha ujauzito, afya za kizazi kijacho chake kitanufaika, hasa kizazi kijacho cha kiume.
Watafiti wa chuo kikuu cha New South Wales wamesema, waliwalisha panya jike kwa chakula chenye mafuta mengi katika wiki sita kabla ya ngono, kipindi cha ujauzito, kipindi cha kunyonyesha. Nusu ya panya hao jike walifanya mazoezi kuanzia siku kumi kabla ya ngono hadi kuzaa panya mchanga, na panya wengine hawakufanya mazoezi. Siku 19 baada ya kuzaliwa kwa panya wachanga, panya hao wachanga watapimwa afya.
Matokeo yanaonesha kuwa, mazoezi yanaweza kupunguza hatari zinazolewa na unene wa wajawazito kwa watoto, kama vile hatari ya ugonjwa wa kisukari wa aina ya II. Jambo lingine linawavitia watafiti ni kwamba, athari hizo nzuri zilioneshwa kidhahiri zaidi katika kizazi kijacho cha kiume. Lakini watafiti hao bado hawajafahamu chanzo cha tofauti kati ya jisia.
Ingawa hilo bado ni jaribio la wanyama, lakini watafiti wameshauri kuwa mazoezi wanayoyafanya wajawazito yatanufaisha afya za watoto.
0 comments:
Chapisha Maoni