Watu zaidi ya 3,000 katika kata ya Tindiga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro hawana pa kuishi baada ya nyumba zao zaidi ya 600 kusombwa na maji huku zingine zikizingirwa na maji kufwatia mafuriko makubwa yaliyo sababishwa na mvua zinazo endelea kunyesha na kusababisha baadhi ya watu kuishi chini ya miti.
Wakizungumza kwa masikitiko wahanga hao wamesema mafuriko yamesababisha waishi katika mazingira magumu ambapo wamesema mafuriko hayo yamevikumba vijiji vitatu huku wakiiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwasaidi kwani hadi sasa watoto hawaendi shule kufuatia nguo na madaftari kusombwa na maji.
Nao viongozi wa kijiji akiwemo diwani wa kata ya Tindiga Yahaya Mbachi wameiomba serikali kuwasaidia wahanga hao kwa vyakula, mahema mavazi pamoja na madawa ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko huku wakimshukuru mbunge wa jimbo la Mikumi kuanza kutoa misaada mbalimbali na kuiomba serikali na taasisi mbali kuona umuhimu wa kuwasaidia kwakuwa wapo katika kipindi kigumu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mikumi Joseph Haule amesema jitahada za kuwanusuru wahanga hao zinaendelea kufanyika na kwamba tayaria amewasilisha maombi ya kupatiwa tani 200 za msaada wachakula huku akitoa wito kwa mashirika, taasisi na makampuni mbalimbali kushirikiana na serikali katika hatua zinazoendelea za kuwanusuru wahanga hao.
0 comments:
Chapisha Maoni