Jumanne, Februari 09, 2016

MFUMUKO WA BEI WASHUKA KWA 0.3% TANZANIA

Shirika linalosimamia takwimu nchini Tanzania (NBS) limesema kuwa mfumuko wa bei nchini umepungua kwa kiasi cha asilimia 0.3, na kufikia asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.8, kati ya mwezi wa Desemba mwaka uliopita na January mwaka huu.
Shirika hilo limesema kuwa upungufu huo umesababishwa na bei ya chini ya mazao mwezi wa Januari mwaka huu ikilinganishwa na Desemba mwaka wa 2015. 
Ephraim Kwesigabo, mkurugenzi mkuu wa sensa ya idadi ya watu na takwimu za jamii katika shirika la NBS, alisema kuwa mfumuko wa kila mwaka wa bei ya chakula na vinywaji visivyo na pombe ilipungua kwa asilimia 10.7 mwezi Januari kutoka asilimia 11.1 mwezi Desemba mwaka 2015.

0 comments:

Chapisha Maoni