Jumatatu, Februari 01, 2016

WAVAMIZI WAVUNJA MSIKITI NA VIBANDA VYA BIASHARA UNGUJA

Watu  wasiojulikana wamevamia katika makazi ya watu eneo la Msumbiji mjini Unguja na kuvunja mabanda na msikiti.
Watu hao maarufu kama mazombi, walifanya uhalifu huo usiku wa kuamkia jana, ambapo walivamia eneo hilo wakiwa wamejifunika nyuso zao na soksi maalumu, huku wakiwa na silaha za jadi.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, amesema  kuwa watu hao walivamia eneo hilo saa 10 alfajiri.
Alisema watu hao baada ya kufika katika eneo hilo, walianza kuvunja mabanda ya mafundi seremala.

0 comments:

Chapisha Maoni