Jumatatu, Februari 01, 2016

TUMWITE SHABIKI NAMBA MOJA WA MESSI?

Kijana wa umri wa miaka 5, raia wa Afghanistan amevutia wengi katika mtandao wa internet nchini China baada ya kuvalia mfuko wa karatasi kuiga jezi ya mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Picha zake kijana huyo akiwa amevalia jezi ya mfuko wa karatasi imesambaa mtandaoni kwa wiki 2 sasa. Shabiki huyo mchanga wa Messi ametambuliwa kama Murtaza Ahmadi na anaishi katika kijiji kimoja kilichoko mkoa wa Ghazni, kusini magharibi ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

0 comments:

Chapisha Maoni