Jumatatu, Februari 01, 2016

UGANDA INAKUWA NCHI YA KWANZA AFRIKA KUTENGENEZA BASI LA MIALE YA JUA BADALA YA MAFUTA

Uganda itakuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kutengeneza basi linalotumia miyale ya jua badala ya mafuta.
Ujenzi wa basi hilo litakalobeba abiria 37 tayari unaendelea katika kiwanda cha kampuni ya Kiira Motors, nchini Uganda. Basi hilo lililopewa jina "Kayoola" litakuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 80 likitumia miyale ya jua au nguvu ya umeme zilizohifadhiwa kwenye betri zake. Basi la "Kayoola" litazinduliwa kati kati ya mwezi huu wa February.

0 comments:

Chapisha Maoni