Alhamisi, Februari 11, 2016

WATOTO WATAKAOZALIWA CHINA MWAKA HUU KUWA NA AKILI KAMA TUMBILI

Huku sherehe za mwaka mpya wa kichina zikiendelea, wanawake waja wazito watakaojifungua mwaka huu wanatarajia kupata watoto werevu na wenye ujasiri "kama tumbili".
Kitamaduni, wachina wanaamini kuwa tumbili ni mnyama mwerevu na jasiri na hivyo basi watoto watakaozaliwa mwaka huu wataridhi sifa hizo.
Hii ni kwa sababu katika tamaduni za wachina, tumbili anaaminika kuwa mnyama wa kupendeza na aliye na sifa kama za binadamu.
Kuna wanyama 12 walioteuliwa kutumika kama ishara ya kila mwaka mpya wa kichina, huu mwaka ukiwa wa tumbili.
Kati ya wanyama hao joka, farasi na tumbili wanaaminika na wachina kuwa na sifa za kupendeza zaidi.
Kufutiliwa mbali kwa sheria ya mtoto mmoja kwa kila familia nchini China kunatarajiwa kuwapa nafasi wanandoa nafasi ya kupata mtoto wa pili, hasa huu mwaka.

0 comments:

Chapisha Maoni