Ijumaa, Februari 26, 2016

UWEZO WA UBONGO WA BINADAMU UNATOFAUTIANA KUFUATIA MABADILIKO YA MAJIRA

Utafiti huo ulifanywa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Liege cha Ubelgiji miaka miwili iliyopita. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa ubongo wa binadamu una uwezo mkubwa zaidi wa kukumbuka katika majira ya mpukutiko (autumn), na uwezo huo ni mdogo zaidi katika majira ya chipukizi (spring). 
Uwezo wa kuzingatia ni mkubwa katika majira ya joto na ni mdogo zaidi katika majira ya baridi. Mchana ni mfupi zaidi katika majira ya baridi, hivyo ubongo wetu hauna haja ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuzingatia mambo mbalimbali.
Watafiti hao wanaona kuwa uwezo wa ubongo unabadilika ili kuendana na hali tofauti ya hewa. Hisia ya binadamu hubadilikabadilika katika majira tofauti, mabadiliko hayo huenda yanaonesha mabadiliko ya ubongo wetu.

0 comments:

Chapisha Maoni