Baadhi ya wanyama wana uwezo wa kuhisi uga sumaku (magnetic field) wa
dunia. Hivi karibuni wanasayansi wa Ulaya wamegundua kuwa molekuli
zinazowasaidia wanyama kuhisi uga sumaku pia ziko katika macho ya mbwa
na baadhi ya nyani.
Molekuli zinazowasaidia wanyama kuhisi uga sumaku zinaitwa Cryptochromes. Ziko ndani ya miili ya vijidudu, mimea na baadhi ya wanyama, wakiwemo ndege, wadudu, samaki na wanyama wanaotambaa. Wanyama hao wanatambua upande, urefu kutoka usawa wa bahari na mahali walipo kupitia uga sumaku. Binadamu hawana uwezo huo.
Watafiti wa taasisi ya Max Planck wakishirikiana na watafiti wa idara nyingine wamegundua kwamba Cryptochromes ziko ndani ya macho ya aina 90 ya mamalia. Molekuli hizi ziko ndani ya macho ya mbwa, mbwa mwitu, mbweha n.k., lakini hazipo kwenye macho ya paka, simba na chui.

0 comments:
Chapisha Maoni