Daktari wa hospitali ya Mayo ya jimbo la Minnesota, Marekani ametoa ripoti ya utafiti akisema, kitambi kina hatari kubwa zaidi kuliko unene.
Ripoti hiyo imesema, kutokana na takwimu za wagonjwa elfu 15, hatari ya kufariki ya wanaume wenye vitambi ni maradufu ya wanaume wanene wa kawaida, na hatari ya kufariki kwa wanawake wenye vitambi ni mara 1.5 ya ile ya wanawake wanene wa kawaida.
Chanzo cha ongezeko la hatari hiyo ni kuwa kitambi kinaweza kuongeza mafuta ndani ya mwili, na maini yatayabadilisha mafuta hayo kuwa lehemu (cholesterol). Lehemu hiyo inaingia katika mishipa ya damu na kusababisha kiharusi na magonjwa ya moyo.
Utafiti wa awali pia ulionesha kitambi kinaongeza hatari ya ugonjwa wa kisukari, kiharusi, magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo na ubongo.
0 comments:
Chapisha Maoni