Jumatano, Februari 24, 2016

TRAFIKI DAR ES SALAAM WAINGIZA TSH. 1.9 BILIONI

Kikosi cha usalama barabarani Kanda maalumu ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi BILIONI MOJA NUKTA TISA 1.9 kutokana na faini za ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia siku ya kwanza ya February 2016 mpaka tarehe 22 February 2016.
Taarifa yao imekuja siku moja baada ya Wizara ya fedha kutangaza jana kukusanya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya TRILIONI MOJA kwa mwezi February 2016 pekee ambao bado haujamalizika kikiwa ni kiwango tofauti na mwaka uliopita ambapo walikua wakikusanya kwenye BILIONI 800 n.k.

0 comments:

Chapisha Maoni