Jumatano, Februari 10, 2016

TANZANIA KUUNDA KITENGO MAALUMU KUPAMBANA NA UJANGILI

Serikali ya Tanzania itaunda kitengo maalum cha kupambana na uwandaji haramu wa wanyamapori, Profesa Abdallah Maghembe, waziri wa maliasili na utalii alisema jana (Jumanne).
Hatua hiyo inajiri wiki mbili baada ya wawindaji haramu kupiga risasi na kuangusha ndege ya helicopter iliyokuwa ikipiga doria katika hifadhi ya Maswa, kusini ya mbuga ya taifa ya Serengeti.
Hadi sasa watu tisa wametiwa mbaroni kuhusiana na kisa hicho ambapo rubani Roger Gower kutoka Uingereza aliuawa.
"Hii ni mojawapo tu ya hatua ambazo zinachukuliwa na serikali ya Tanzania kuimarisha vita dhidi ya uwindaji haramu na uporaji wa maliasili," Profesa Maghembe alisema.

0 comments:

Chapisha Maoni