Jumatano, Februari 03, 2016

SHEHE PONDA AMKUMBUSHA RAIS MAGUFULI SUALA LA ZANZIBAR

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Issa Ponda amemkumbusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.
Ametoa kauli hiyo leo katika Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari juu ya namna Dk.Magufuli anavyoweza kutatua mgogoro huo ili kuzuia machafuko kwani kuna viashiria vya machafuko kipindi hiki.
Ponda alisema Rais Magufuli anao wajibu wa kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati akihutubia Bunge kuwa ndio suluhisho la mgogoro huo wa kisiasa pasipo kusababisha Zanzibar kuingia katika dhiki na uhasama uliopitiliza.
Aidha, alisema msajili wa vyama vya siasa nchini pia anaweza kuingilia kati mgogoro huo kwani anayo mamlaka ya kuwakutanisha viongozi wa kisiasa wa pande mbili za CCM na Cuf kwa kukaa na kutafuta suluhu ya mzozo huo.

0 comments:

Chapisha Maoni