Alhamisi, Februari 25, 2016

NAIBU SPIKA, TULIA AKSON ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI MBEYA

Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, dk. Tulia Akson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali Kiwira mkoani hapa.
Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria kugongana na gari dogo lililokuwa na abiria sita wa familia moja katika eneo hilo la Kiwira 
Taarifa zinasema hakuna kifo kilichotokea kutokana na ajali hiyo japokuwa majeruhi wengi ambao ni watoto wanne walipatikana katika gari lililogongana na gari la mhe. Naibu spika.
Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, dk. Tulia akson alikuwa akitokea hapa jijini Mbeya ambapo alikuwa na ziara binafsi katika shule ya sekondari ya wasichana ya Loleza ambapo alisoma elimu yake ya kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1991 hadi 1994.
Katika ziara hiyo naibu spika tulia akson alitoa msaada wa pesa za kitanzania milioni 5 kwaajili ya ukarabati wa bweni alilokuwa akilitumia wakati akisoma shuleni hapo.

0 comments:

Chapisha Maoni