Jumatatu, Februari 08, 2016

MKE WA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU PINDA APATA AJALI ILIYOUA MMOJA NA KUJERUHI WANNE


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe anaelezea kuhusiana na ajali hiyo.
Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni