Jumatatu, Februari 08, 2016

IS WANYONGA WATU 300 IRAQ

Kundi la kigaidi la Islamic State (IS) limeripotiwa kuwanyonga zaidi ya watu 300 siku chache zilizopita katika mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq.
"Waliouawa ni maafisa waliostaafu wa polisi na jeshi pamoja na wanaharakati ambao walisemekana kushirikiana na serikali ya Iraq," Mahmoud Soorchi, msemaji wa shirika moja linaloendesha kampeni ya kukomboa mji wa Mosul kutoka mkononi mwa IS aliambia waandishi wa habari. Mji wa Mosul umekuwa chini ya udhibiti wa IS tangu mwezi wa sita mwaka wa 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni