Jumatano, Februari 10, 2016

MAAJABU YA SIKU 100 ZA DKT MAGUFULI

Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliingia ofisini Novemba 5,2015 akiwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt Magufuli ndani ya siku hizi takribani 100 amejizolea umaarufu mkubwa mitandaoni na duniani Kwa wananchi waliowengi Kwa namna anavyochapa Kazi unaonogeshwa na kauli mbiu yake ya HAPA KAZI TU!
Dkt Magufuli ameonekana kujikita zaidi katika kushughulikia matatizo ya msingi ya nchi hasa vitendo vya ufisadi wa rasilimali za Taifa, Ubanaji wa matumizi serikalini, upatikanaji wa huduma za jamii, uimarishaji wa miundombinu, kuzuia ukwepaji kodi TRA na TPA n.k
MAAJABU YA SIKU 100 ZA DKT MAGUFULI
1. Alifuta vitengo vya mapokezi na lishe Ikulu punde baada ya kuingia ofisini na kuwarejesha watendaji husika katika wizara mama walizotoka.
2. Aliweka mkazo katika kuzuia na kupambana na ukwepaji kodi TRA na TPA ili kuongeza ukusanyaji mapato. Hapa vigogo kadhaa walionekana hawatamudu kasi ya HAPA KAZI TU walisimamishwa Kwa uchunguzi na wengine kufukuzwa huku hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi yao.
3. Kubana matumizi ili kuhakikisha serikali inapata fedha za kuendesha miradi ya maendeleo, kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma Kwa wananchi waliowengi. Mifano ya Ubanaji matumizi ni:-
(a) Aliagiza zaidi ya shilingi million 200 zilizokuwa zitumike katika hafla ya uzinduzi wa bunge zikatumike kununulia vitanda vya wagonjwa hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili ambapo vitanda 300 vilinunuliwa.
(b) Alifuta shamrashamra za maadhimisho ya sherehe za uhuru wa (Tanganyika) Tanzania Bara Disemba 9, 2015 ambapo aliokoa shilingi billion 4.2 fedha zilizoelekezwa kufanya upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge ambao unaendelea.
(c) Amepiga marufuku safari za nje Kwa mawaziri, viongozi waandamizi wa serikali na hata katika mashirika ya umma pasipo kibali cha Ikulu huku akiagiza mabalozi wa Tanzania katika nchi husika kuiwakilisha serikali yake huko. Katika eneo hili ameokoa zaidi ya shilingi billion 3.5 Kwa kuacha kusafiri safari tano ambazo ni:-
(i) Novemba 27,2015 mkutano wa wakuu wa nchi wa jumuiya ya madola (CHOGM) uliofanyika visiwa vya Malta. Badala yake Tanzania iliwakilishwa na balozi wa Tanzania Uingereza na maafisa watatu.
(ii) Novemba 29, 2015 mkutano wa kimataifa wa 21 wa kujadili mabadiliko ya tabianchi Duniani (COP21) uliofanyika Paris, ufaransa. Ulihudhuriwa na Marais 150 kati ya 195 wakiwamo Barack Obama na Xi Jinping. Tanzania iliwakilishwa na balozi.
(iii) Disemba 5, 2015 mkutano wa tano wa wakuu wa nchi wa Afrika na Rais wa China Xi Jinping kupitia jukwaa la nchi za Afrika na China (FOCAC). Tanzania ilihali na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
(iv) Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa makuu (SADC) uliofanyika Gaborone, Botswana. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Ndg Majaliwa Kassim Majaliwa.
(v) Mkutano wa Umoja Wa Afrika (AU) uliowakutanisha wakuu wa nchi za Afrika ulifanyika Addis Ababa, Ethiopia. Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Balozi Agustine Mahiga.
Katika kuonesha hana masihara na agizo hili serikali iliwasimamisha Kazi watumishi wanne wa TAKUKURU Kwa kwenda nje ya nchi pasipo kibali maalum cha Ikulu.
Fahamu msafara wa Rais wa JMT kwenda nje ya nchi huwa na Watu kuanzia 50 ambapo huitajika zaidi ya million 700 kuwahudumia
Dkt Magufuli amesafiri nje ya Dar es Salaam mara 5 huku akiwa amepanda ndege mara mbili tu!
4. Aliapisha baraza la mawaziri na wateule wake wakiwamo makatibu wakuu wa wizara na manaibu wao bila shamrashamra wala mbwembwe kama ilivyozoeleka huku wahusika wakifika Ikulu kuapa bila kuambatana na utitiri wa ndugu na jamaa ambao wangewalaki Kwa maua na mashada baada ya kuapishwa.
5. Amefuta umiliki wa mashamba 17 makubwa ambayo hayaendelezwa na kuyarejesha serikalini.
6. Wananchi wa mataifa mengi Duniani wanapaza sauti kila kukicha wakizitaka serikali zao kumuiga Dkt Magufuli mfano Australia walimtaka waziri mkuu wao kumuiga katika kubana matumizi.

1 comments: