Jumamosi, Februari 13, 2016

LEO KATIKA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA

  • Mshikemshike wa ligi kuu Tanzania bara utaendelea tena wikiendi hii ambapo jumamosi kutapigwa jumla ya michezo mitano.
  • Stand United watakua wenyeji wa Wekundu wa msimbazi Simba Sport klabu, huku Mgambo Jkt wakipimana ubavu na African Sport.
  • Mbeya City wao watakua katika dimba lao la sokoine mjini Mbeya, kuwaalika wanakishamapanda timu ya Toto Afrikans toka Mkoani Mwanza.
  • Majimaji watakuwa wageni wa Ndanda Fc mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Nangwanda sijaona huko mkoani mtwara, Jkt Ruvu watakipiga na Kagera Sugar.
  • Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa michezo miwili kuchezwa Mwadui Fc watapima ubavu na Tanzania Prisons, huku Coastal Union wakiwaalika Azam Fc.

0 comments:

Chapisha Maoni