KLABU ya soka ya Mbeya city FC ya jijini hapa jana imeingia mkatabu wa miaka mitatu na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Malawi ‘the Fl”mes", Kinnah Phiri kwa ajili ya kukinoa kiosi hicho.
Hafla ya kuingia mkataba huo ilifanyika jana katika ofisi ya Meya wa jiji na kati ya Meya David Mwashilindi, Kaimu Mkurugenzi jiji Samwel Razaro na Mwenyekiti wa timu hiyo Mussa Mapunda.
Akizungumza na kabla ya kuingia mtabata na kocha huyo Katibu wa timu hiyo Emmanuel Kimbe alisema kuwa mchakato wa kusaka kocha ulianza tangu mwaka jana na kuanza naye mazungumzo na hatimaye mwaka huu amekubali kuinguia mkataba wa miaka mitatu kuanzi Februal mwaka huu.
Akizungumzia uwezo wa Kocha huyo Kimbe alisema kuwa wadau wa wapenzi wa klabu hiyo wasiwe na hofu na kocha huyo kwani uwezo wake si wa kutiliwa shaka kutokana na kuwa amekuwa mwalimu na soka katika klabu mbali mbali ikiwemo timu ya Taifa ya Malawi kuileta mafanikio makubwa akiwa kocha mazawa.
Akizungumzia hatima ya kocha aliyekuwa akiinoa timu hiyo Abdul Mingane, Kimbe alisema klabu hiyo haija vunja mkataba kamba ambavyo imeripotiwa na kwamba bado ni mtumishi harali na mara baada ya kumaliza matatizo yake ya kifalimilia atarejea .
‘Sisi hatuja vunja mkataba na Mingane bali aliaga kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo atakapokuwa tayari ataungana na sisi na kwamba hata mkataba wa kwanza hakuajiliwa kama kocha Mkuu hivyo bado ni mtumishi wa jijji’ aliongeza Kimbe
Kwa upande kocha Phiri alisema kuwa yeye siyo mgeni katika soka la Tanzania na kwamba anatambua vyema kiu ya wapenda soka katika jiji la Mbeya na Tanzania kwa ujumla hivyo watarajie mambo makubwa kutoka kwake.
Amesema kuwa licha ya wanambeya kuwa ya kiu kiu kubwa ya mafanikio lakini yote hayo yatapatikana kwea ushirikiano na anahitaji ushirikiano mkubwa kwa wadau wote wa soka katika jiji la Mbeya wakiwemo mashabiki, viongozi na wapenzi wa mchezo huo.
Natambua kazi niliyo nayo lakini kiu ya wanambeya ni kuona timu yao inafanya vizuri lakini ni vema watambue wazi kuwa mafanikio ya timu hayaletwi na kocha pekee yake bali kwa ushirikiano mzuri wa Kocha,Benchi la Ufundi, Viongozi wa klabu, wachezaji lakini pia mashabiki na nina imani nitapata ushirikiano kutoka mzuri kutoka kwao’ alisema Phiri
Kocha huyo ambaye alishuhudia mchezo baina ya timu hiyo na Tanzania Prisons ulipigwa Februal 7 mwaka huu katika dimba la Sokoine na kutoka sare ya bila kufungana,alisema kuwa kikosi hicho kipo vizuri ipo katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.
Kwa upande wake Meya bwa jiji la Mbeya Dedid Mwashilindi alisema kuwa kutoka na uwezo wa kocha huyo wanamatarajio makubwa kuwa ataleta mabadiliko ya soka na hasa kutokana na maelezo yake kuwa yeye ni muumini mkubwa wa soka la vijana.
Amesema kuwa ni vema kocha huyo akatambua kuwa matarajio ya wanambeya ni kuona inabadilika kutokana na kuwa hivi karibuni imekuwa na matokea mabaya huku akiwaomba wadau wa soka kumpa muda kocha huyo na kumuonyesha uhirikiano wakati akitekeleza majukumu yake.
Phiri ana kuwa kocha wa tatu kuionoa timu hiyo tangu ipande daraja mwaka 2013 huku akiwa kocha wa kwanza mgeni kuanza kukinoa kikosi ambacho kimekuwa na matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni kwana mpaka sasa inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu ikiwa imecheza michezo 18 sare 8 kushinmda minne na kufungwa na kufungwa sita.
0 comments:
Chapisha Maoni