Ijumaa, Februari 12, 2016

KIPINDUPINDU CHAIPELEKA HELIKOPTA YA POLISI IRINGA

Inakadiriwa kuwa takribani watu 3000 wakiwemo wagonjwa wa kipindupindu wamefungiwa na Maji ya Mto Ruaha Mdogo yaliyohama mkondo wake na kutengeneza njia tofauti tatu. 
Watu hao ambao wengi wao wapo vitongoji tofauti vitatu vya kilimo ya mashamba makubwa ya mpunga Tarafa ya Pawaga Iringa vijijini, hawajala chochote kwa siku pili leo kutokana na kutokuwepo kwa njia ya kuwapelekea chakula kama awali. 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Amina Masenza, Mchana huu amekiri hali hiyo na kueleza kuwa wameomba Helikopta ya Polisi kwa lengo la kwenda kudondosha chakula maeneo hayo ambayo yamegeuka kama bahari baada ya kujaa maji lakini pia kuanza kuwaokoa. 

Yonna Mgaya- Iringa

0 comments:

Chapisha Maoni