Watafiti wa Marekani wanasema, chakula cha nchi za magharibi kinaweza kusababisha madhara ya ini, lakini madhara hayo yanaweza kuondolewa kwa kupunguza sukari na mafuta kwenye chakula.
Watafiti wa chuo kikuu cha Oregon wanasema, chakula cha nchi za magharibi kinakuwa na sukuri nyingi, mafuta mengi na lehemu nyingi, vitu ambavyo vinasababisha madhara kwa maini ama hata kusababisha saratani.
Imefahamika kwamba, nchini Marekani kiwango cha maradhi ya maini yasiyohusiana na pombe kinaongezeka kwa kasi sana, ambacho kinahusisha asilimia 10 hadi 35 ya watu wazima na watoto.
Kutokana na takwimu za majaribio yaliyofanywa kwa wanyama, kupunguza mafuta na lehemu kwenye chakula kunaweza kupunguza uzito wa mwili na kuboresha umetaboli, na hali ya afya ya ini huboreka.
Dkt Kelly Lytle aliyeshiriki kwenye utafiti huo amesema, walijaribu kutumia chakula chenye mafuta machache kuondoa tatizo la madhara ya ini, lakini wakagundua kuwa ili kuongeza ladha ya chakula chenye mafuta machache, chakula hicho kinatiwa sukari nyingi.
Hivyo, watafiti wanashauri kuwa, ili kuboresha afya ya ini, wagonjwa wanatakiwa kupunguza ulaji wa sukari kuboresha mtindo wa chakula na kufanya mazoezi zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni