Alhamisi, Februari 11, 2016

AJALI YA BASI YAUA 11 TANGA

WATU 11 wamefariki dunia huku wengine 26 wakijeruhiwa, wanne kati yao wakiwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga, kutokana na ajali ya gari.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 1 asubuhi katika eneo la Tanga Mlima mkoani Tanga, iliyohusisha basi la kampuni ya Simba Mtoto lenye namba za usajili T 393 DBZ na lori aina ya Scania lenye namba T 738 CFE ambalo lilikuwa limebeba mchanga.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kusinzia na kuhama njia, kulikopelekea kwenda kugongana na basi hilo lililokuwa likitoka mkoani Tanga.
Kamanda Msikhela amesema majeruhi hao kwa sasa wako hospitali ya Muheza na 24 kati yao wanaendelea vizuri, huku watu 11 waliofariki, wanaume nane na wanawake watatu, akiwemo mtoto wa miaka miwili na nusu wote wakiwa wa familia moja.

  • Tuma sms NIUNGE katika namba yetu ya whatsapp tukuunganishe na mtandao wetu katika group la WHATSAPP

0 comments:

Chapisha Maoni