Chelsea wanamtaka meneja wa Italy Antonio Conte, 46, awe meneja wa muda mrefu kuziba nafasi ya Jose Mourinho (Mail), Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa CSKA Moscow, Ahmed Musa, 23, ambaye pia anasakwa na Leicester (Express), beki wa Chelsea Gary Cahill anasakwa na Roma (London Evening Standard), meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anafikiria kumsajili kiungo wa Udinese, Pior Zielinski, 21 (Mirror), mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 23, amesema angependa kucheza chini ya Pep Guardiola. Meneja huyo anatarajiwa kwenda Manchester City mwisho wa msimu (Mirror), West Brom wanazungumza na QPR kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa zamani wa Tottenham, Sandro (Telegraph), beki wa New York Red Bulls, Matt Miazga, 20, alikuwa London siku ya lhamisi ili kufanya vipimo vya afya Chelsea (Sky Sports), dau la Arsenal la kumtaka Ben Chilwell, 19 kutoka Leicester, limekataliwa (Football Insider), Newcastle United huenda wakaacha kumfuatilia Saido Berahino, 22, licha ya kuwa tayari kutoa zaidi ya pauni milioni 20, lakini West Brom wana 'dengua' (Newcastle Chronicle), Newcastle huenda wakaamua kumfuatilia Loic Remy, 29, wakimkosa Berahino (Telegraph), West Ham na Norwich wanataka kumsajili beki wa Inter Milan, Davide Santon, 25 kwa mkopo (Mail), uhamisho wa kiungo wa West Ham Reece Oxford, 17, kwenda Charlton umekwama kwa sababu meneja wa Charlton Jose Riga hajawahi kumsikia (Sun), mwekezaji Mmarekani wa Bournemouth Matt Hulsizer, amesema meneja wake Eddie Howe haendi popote. Howe, 38, amekuwa akihusishwa na kwenda Chelsea baada ya Guus Hiddink kuondoka (Daily Echo), Manchester United wana matumaini ya kumsajili kiungo kutoka Ureno, Domingos Quina, 16, anayeichezea Chelsea (Sun), meneja wa Sunderland, Sam Allardyce amesema ana orodha ya majina 60 ya wachezaji anaowataka (Newcastle Chronicle), meneja wa Crystal Palace, Alan Pardew ana wasiwasi kuwa Emmanuel Adebayor, 31, ataondoka mwisho wa msimu (Star). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye magazeti ya Ulaya. Zimebaki siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa
Salim Kikeke
0 comments:
Chapisha Maoni