Hatimaye leo mchezaji kutoka Tanzania, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars
Mbwana Samatta
ameingia mkataba rasmi na Club yake mpya ya FC Genk. Mbwana Samatta ametambulishwa kwa waandishi wa habari leo nchini Ubelgiji baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo inayocheza katika Ligi kuu ya nchini humo.
Mbwana Samatta alisema kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa; "Kama mnavyojua Ubelgiji ndio imekuwa chanzo kikubwa cha wachezaji wengi wakubwa na kikosi chao cha timu ya Taifa ni moja kati ya timu bora duniani. Namshukuru Mungu kwa fursa hii na nitaitumia ipasavyo. #HainaKufeli #LetsGo #TeamGenk #Timu ya Tanzania"
0 comments:
Chapisha Maoni