Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www. kenya-today .com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii.
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanahabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko Watanzania wenyewe.
Haijulikani ni nini hasa nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo .
Taarifa hiyo si ya kweli.
0 comments:
Chapisha Maoni