Jumatatu, Januari 11, 2016

WAZIRI: TUKIO LA UBAKAJI WA WANAWAKE 90 SIKU YA MWAKA MPYA LILIPANGWA

Waziri wa sheria nchini Ujerumani Heiko Maas amesema anaamini kuwa visa vya juzi vya unyanyasaji wa kijinsia katika mji wa Cologne vilipangwa. 
Kundi la wanaume wapatao 1,000 wenye asili ya kiarabu na Afrika kaskazini walizingira na kudhulumu kijinsia wanawake katika mji wa Cologne ulioko magharibi ya Ujerumani wakati wa sherehe za mwaka mpya. Wanawake wapatao 90 waliripotiwa kunyanyaswa kingono kwenye kisa hicho huku watu wengine wengi wakiripoti kuibiwa mali.

0 comments:

Chapisha Maoni