Jumapili, Januari 24, 2016

VITA YA MANENO KATI YA WANACCM NA MEMBE

Mbunge wa Nzenga Mjini (CCM), Hussein Bashe amemtaka aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuacha kumshambulia Rais John Magufuli katika utendaji wake.
Kauli ya Bashe imekuja siku moja baada ya mfululizo wa habari zilizomnukuu Membe akimkosoa Rais Magufuli katika maeneo kadhaa likiwamo suala la kuzuia safari za nje, Rais kwenda nje ya nchi huku akimpa tahadhari ya kuwashughulikia wafanyabiashara wakubwa.
Kupitia taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, Bashe alisema Membe amekuwa waziri kwa miaka kumi na kutimiza wajibu wake, hivyo amuache Magufuli naye atimize wajibu wake kwa wananchi.

0 comments:

Chapisha Maoni