RAPA wa Philly asiyeishiwa skendo nchini Marekani Meek Mill, jana Ijumaa alitangaza kujiunga na chuo cha Overbrook High School iliyopo kitaani kwake.
Mill alipta nafasi ya kupanda jukwaani na kutoa hamasa kwa wanafunzi waendelee kubaki shuleni na vyuoni wakisoma ili wajiendeleze kielimu na kimaarifa pia.
“Nimeamua kujiunga na chuo mimi mwenyewe,” alisema Meek. “Nimechukua uamuzi huo mimi mwenyewe kwa sababu ninataka kuwa bora zaidi kwa kile ninachokifanya. Ninataka kuwa bora zaidi kwa kile ninachokifanya ndiyo maana nimejiunga na chuo kujielimisha mwenyewe, kupata elimu zaidi ya hii niliyonayo kwa sababu elimu inatengeza pesa, ukielimika utapata pesa nyingi, na ninapenda kutengeneza pesa na kuijali familia yangu.”
Wakati akitoa hamasa hiyo, Meek aliwaambia wanafunzi hao kuwekeza muda wao kwa kufanya vitu ambavyo vina manufaa katika maisha yao. “DC4, Nicki Minaj, Drake hawatengenezi mkwanja” alitania Meekl.
“Nilipokuwa na umri kama wa kwenu hivi, sikupata nafasi ya kuzungumza na Jay Z, sikupata nafasi ya kuzungumza na Beanie Sigel, ili niwaulize nitafikiaje mafanikio waliyo nayo wao?”
Meek anasubiria Februari 5 kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka baada ya kukiuka masharti ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichonacho.
Kwa sasa Meek haruhusiwi kusafiri nje ya nchi wala kufanya shoo nje ya Philly.
0 comments:
Chapisha Maoni