Alhamisi, Januari 28, 2016

VIDEO; J. MAKAMBA; MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR NI HALALI

Waziri wa Mazingira na Muungano, January Makamba amesema kuwa Tangazo la Kufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar lilitolewa na Tume ya Uchaguzi visiwani humo lilikuwa halali na kwa mujibu wa sheria.
Makamba amesema kwenye kikao cha tume cha tarehe 21 January cha kuamua 
kuatangazwa kuamua kurudiwa kwa uchaguzi, akidi ilitimia na wengi walikubaliana na uamuzi ule, kwa hio uamuzi ni halali kisheria na kikatiba na katiba ya Zanzibar inasema hakuna mwenye mamlaka hata mahakama ya kuhoji au kuchunguza maamuzi yanayotolewa na tume kuhusu uchaguzi.
Amesema hayo Bungeni wakati akitoa ufafanuzi Bungeni kuhusu Mkwamo wa Kisiasa unaoendelea Visiwani Zanzibar.

0 comments:

Chapisha Maoni