Watafiti wa chuo kikuu cha Sao Paulo cha Brazil wamegundua kuwa ulaji wa chakula chenye mafuta mengi una uhusiano mkubwa na wasiwasi na mfadhaiko.
Katika majaribio ya mfululizo, watafiti waliwalisha panya weupe chakula chenye mafuta mengi na baadaye uzito wa panya hao ukaongezeka huku kiwango cha sukari kwenye damu pia kikiongezeka. Mbali na mabadiliko hayo, panya hao pia walionesha dalili za wasiwasi na mfadhaiko. Ingawa watafiti walitumia dawa kuwatibu panya hao, lakini dalili hizo hazikutoweka.
Wakati watafiti hao waliposimama kuwalisha panya hao chakula chenye mafuta mengi, baadala yake panya hao walikula chakula cha kiafya. Baada ya hapo, hali ya wasiwasi na mfadhaiko ya panya inapungua na uzito wao ulipungua na kiwango cha sukari katika damu pia kilirudi katika hali ya kawaida.
Watafiti pia wanashauri kuwa daktari wa tiba ya magonjwa ya akili wasiwapatie wagonjwa dawa zinazoweza kuvuruga uwiano wa umetaboli wa mwili wa binadamu.
0 comments:
Chapisha Maoni