Jumamosi, Januari 16, 2016

UKAWA WASHINDA UMEYA ILALA NA KINONDONI

Uchaguzi wa meya wa halmashauri wa Ilala jijini Dar es Salaam umefanyika  ambapo Charles Kuveko (Chadema) ameshinda umeya Ilala leo kwa kura 31 na Naibu Meya ni Omary Kumbilyamoto (CUF), kura 31 wakati huo huo  leo uchaguzi wa meya wa halmashauri wa Kinondoni  jijini Dar es Salaam umefanyika  ambapo diwani wa Ubungo kutoka UKAWA, Boniface Jacob (CHADEMA) amekuwa meya na na Naibu Meya  ni diwani wa Tandale, Jumanne Amir Mbunju (CUF).
Katika uchaguzi huo, Chadema kilipata kura 38 na CCM kura 20 ambapo katika unaibu meya Cuf  kilipata kura 38 na CCM kura 20.

0 comments:

Chapisha Maoni