Siku kama ya leo miaka 15 iliyopita Rais Laurent Desire Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alipigwa risasi na mmoja wa walinzi
wake katika ikulu ya Rais na kujeruhiwa vibaya. Baada ya tukio hilo
kulienea habari za kutatanisha juu ya hatima ya Rais huyo. Tarehe 18
Januari yaani siku mbili baadaye, serikali ya Kinshasa ilithibitisha
kufariki dunia Rais huyo. Kabila alizaliwa mwaka 1939 huko Katanga
alihudhuria masomo ya Chuo Kikuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Tanzania. Aliingia madarakani mwaka 1997 baada ya vikosi alivyokuwa
akiviongoza kuuteka mji wa Kinshasa, na kupelekea Rais Mobutu Sese Seko
kukimbilia nje ya nchi. Tarehe 26 Januari Joseph Kabila mwana wa Rais
Kabila alishika haramu za uongozi nchini Congo.
0 comments:
Chapisha Maoni