MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma leo imefutilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jonathan Njau kupinga ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu (Chadema).
Njau alishindwa kwenye uchaguzi kwenye jimbo hilo mwaka 2010 na 2015. Njau aliwasilisha ombi mahakamani kwa kutaka kesi hiyo kufutwa kwani hana haja ya kuendelea na shauri hilo.
Awali mlalamikaji aliwahi kupeleka mahakamani mara mbili maombi ya ombi la kusamehewa kwa gharama za kesi kiasi cha milioni 15 lakini maombi hayo yalitupwa na mahakama.
Akizungumza nje ya mahakama baada ya shauri hilo kutupwa Lissu amesema aliweka hoja sita za kupinga uhalali wa kesi hiyo hata angelitoa Sh. milioni 15 angeshindwa kwenye mapingamizi.
“Kesi aliyofungua mwaka 2010 ilikuwa na makosa yale yale hakuna kilichobadilishwa labda jina, tarehe na mwaka,” amesema Lissu na kuongeza:
“Hii kesi ingekuka tu kwa sababu ililetwa bila umakini wowote makosa mbalimbali ya kisheria yalikuwepo hata angelipa milioni 15 angeondolewa tu kwenye pingamizi.
“Hakuna aliyobadilisha, wakati ule alifunguliwa kesi na wapambe wake lakini baadae sheria ikabadilika.
“Narudia rai niliyotoa wiki mbili zilizopita kwenye kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Injinia Christopher Chiza makosa yale yale hawa watu wanafundishana.”
Lissu amesema Mahakama Kuu ilishatamka mwaka 2010 kuwa kesi za uchaguzi si za kuendelea kwa papara bila umakini wowote, bila wakili kutekeleza vitu rahisi rahisi vya kisheria.
“Sipunguziwi kasi mahakamani, kesi za uchaguzi nilianza kufanya miaka 10 iliyopita mtu ambaye alishtakiwana CCM nilisimamia kesi hizo,” amesema Lissu.
0 comments:
Chapisha Maoni