Alhamisi, Januari 21, 2016

TETESI ZA SOKA ULAYA - ALHAMISI 21.01.2016

Chelsea wamekubaliana na Corinthians kumsajili mshambuliaji kutoka Brazil, Alexandre Pato, 26, kwa pauni milioni 8 (Daily Express), Pato yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kujiunga na Chelsea, na amekubali mkataba wa miaka mitatu (Daily Mail), kuwasili kwa Pato huenda ndio ukawa mwisho wa Radamel Falcao, 29, ambaye anacheza Chelsea kwa mkopo na hivyo kurejea Monaco (Guardian), Aston Villa wanazungumza na beki wa zamani wa Manchester United Nemanja Vidic, 34 (Sun), Manchester United wanafikiria kupanda dau kumchukua mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Edinson Cavani, 28, (ESPN), Arsenal wapo tayari kutoa pauni milioni 37 kumsajili kiungo kutoka Uswisi, Granit Xhaka, 23, anayeichezea Borussia Monchenglabach mwisho wa msimu (Daily Star), Xhaka hata alifanya mzaha na waandishi wa habari na kusema amemuomba kiungo wa Arsenal, Francis Coquelin, namba 34 ya jezi anayovaa (London Evening Standard), kiungo wa Chelsea, Pedro, 28, anataka kuondoka Darajani, miezi mitano tu baada ya kujiunga nao akitokea Barcelona kwa pauni milioni 21 (Daily Star), Saido Berahino bado anaendelea kusubiri kuona kama ataruhusiwa na West Brom kuondoka. Berahino anataka kwenda Tottenham, lakini klabu yake inataka kumuuza kwenda Newcastle kwa pauni milioni15 (Daily Mirror), Chelsea hawakuweka kipengele cha faida ya mauzo kwa Romelu Lukaku aliyekwenda Everton, ambaye sasa ana thamani ya pauni milioni 60, akihusishwa na kuhamia Manchester United, Juventus na Real Madrid (Times), Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 9 kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Sandro Ramirez, 20 (Daily Express), beki kutoka Ufaransa, Eliaquim Mangala huenda aligharimu pauni milioni 42 badala ya 32 zilizotajwa awali, hii ni kufuatia nyaraka za uhamisho zilizoonekana (Manchester Evening News), Standard Liege wanataka kumchukua kipa Victor Valdes, 34 kwa mkopo kutoka Manchester United (Daily Mail), meneja wa Sunderland Sam Alardyce yuko tayari kuwapa Swansea Fabio Borini, 24, ili aweze kusamjili Andre Ayew, 26 (Sun), Sunderland wamepoteza matumaini ya kumsajili beki kutoka Ivory Coast Lamine Kone, 26, kutoka Lorient (Sunderland Echo), Real Madrid wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Uruguay, Rodrigo Bentacur, 18, anayeichezea Boca Juniors (Daily Mirror), dau la pauni milioni 7 la Stoke City kumsajili beki wa Burnley Michael Keane, 23, limekataliwa (Metro), West Ham haitomuachilia kiungo wake Pedro Obiang, 23, kuodoka mwezi huu (London Evening Standard), West Ham wana uhakika wa kukamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji Emmanuel Emenike, 28, kutoka Fenerbahce (Daily Telegraph), Newvcastle wamedhamiria kutomuuza kiungo Moussa Sissoko, 26 pamoja na Ayoze Perez, 22, mwezi huu, lakini watakuwa tayari kumuuza Yoan Gouffran, 29 na Sylvain Marveoux, 29 (Newcastle Chronicle), Swansea wamewasiliana na Joe Allen wa Liverpool kutaka kumshawishi arejee Liberty Stadium (Wales Online). Hayo ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye magazeti ya Ulaya.

Salim Kikeke

0 comments:

Chapisha Maoni