Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania amesema kuwa serikali inapanga kutumia njia za kisheria kuwarudisha nyumbani wahajiri haramu kutoka Ethiopia na nchi nyinginezo.
Charles Kitwanga, amesema kuwa, mchakato huo umeanza na kwamba unawalenga wahajiri kutoka nchi kadhaa ambao wako Tanzania kinyume cha sheria.
Polisi ya Tanzania mwezi uliopita iliwakamata raia 40 wa Ethiopia waliokuwa wamewekwa kwenye nyumba moja jijini Dar es Salaam wakisubiri kusafirishwa hadi Afrika Kusini kimagendo.
Kwa muda mrefu sasa, Tanzania imekuwa ikitumiwa na watu wanaoendesha biashara haramu ya magendo ya binadamu kama sehemu ya kuwapitishia wahajiri wa Ethiopia na Somalia kuelekea Afrika Kusini.
Wachambuzi wanasema idadi kubwa ya Waethiopia wanatoroka nchini mwao kutokana na mbinyo wa kisiasa, ukosefu wa ajira na ukame wa muda mrefu.
0 comments:
Chapisha Maoni