Jumanne, Januari 26, 2016

SIMU 2744 ZA STARTIMES ZAKAMAMTWA NA TRA

Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo amethibitisha kukamatwa maboksi 294 yenye simu 2,744, na vifaa mbalimbali vya simu katika ghala la Kampuni ya StarTimes.
Kayombo amesema mamlaka hiyo ilikamata maboksi hayo ambayo thamani yake haijajulikana baada ya kutilia shaka nyaraka za mizigo hiyo iliyoingizwa nchini ikiwa haionyeshi ni ya nani, ilikotoka pamoja na kuwepo kwa taarifa zenye utata kuhusu idadi ya mizigo hiyo.
"Tulipokea taarifa za utata wa mizigo iliyodaiwa kuingizwa na kampuni hiyo jambo lililotulazimu kwenda kuikamata kwa ajili ya uchunguzi.
“Tulikamata maboksi yaliyokuwa na simu na vifaa mbalimbali kama vile betri, chaji za simu, powerbank na kava za simu. Baada ya kuikamata tuligundua kulikuwa na udanganyifu wa idadi ya maboksi yaliyokuwa kwenye nyaraka, kwani zilisomeka kuwa kuna maboksi 211, lakini katika uchunguzi tulikuta 294,” alisema Richard Kayombo.

0 comments:

Chapisha Maoni