Mnyama Simba amevamia Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na kuuwa watu wawili baba na mtoto wake ambapo simba huyo alikula mwili wa mtoto na kuacha kichwa huku na kunyonya damu ya mzazi hadi kupoteza maisha.
Tukio la Simba huyo kuua watu wawili limetokea jana majira ya saa kumi na moja alfajiri katika Kijiji hicho cha Sitalike .
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher Anjelo amewataja waliouawa ni John Jeremia (45) na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka mitano .
Ameeleza baada ya Simba huyo kuingia ndani alimvamia baba wa mtoto huyo na kuanza kumnyonya damu hadi alipohakikisha amefariki nakuhamia kwa mtoto wa marehemu na kumtafuna mpaka kiliposalia kichwa
Alisema taarifa za simba kuua watu hao zilifika kwenye uongozi wa Kijiji hicho ambao nao walitoa taarifa kwa askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambapo walianza kufanya msako wa kumsaka simba huyo kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Sitalike.
Wakati wakifanya msako waliona nyayo za simba na walizifuata kule zilipoelekea na walipofika kwenye kichaka walimuona simba huyo akiwa amekaa na pembeni yake kukiwa na kichwa cha mtoto Mwenyekiti wa Kijiji alisema askari wa Hifadhi ya Katavi walimfyatulia simba huyo risasi lakini aliweza kuikwepa na kusogea mbele zaidi .
Alieleza baada ya Simba huyo kuwa ameuawa kwa kupigwa risasi baadhi ya wananchi waliomba wamchukue kama kitoweo cha mboga lakini askari wa TANAPA waliwakatalia na walimchukua simba huyo aliyekuwa amekufa na kwenda nae kwenye hifadhi yao kwa kile walichoeleza kuwa wanakwenda kumchoma moto kwa kutumia mafuta ya petroli.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kuuawa kwa watu hao na Simba huyo aliyetokea kwenye Hifadhi ya mbuga ya Katavi .
Alisema ameisha peleka askari wake kwenda kuangalia eneo la tukio hilo na ametoa wito kwa wananchi kuacha kujenga makazi karibu na hifadhi ya Katavi.



0 comments:
Chapisha Maoni