Alhamisi, Januari 07, 2016

SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA KUWAONDOA WAGENI NA KUWAPA FURSA WAZAWA

Kufuatia maagizo ya serikali, Naibu waziri wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, mhe. Hamad Yusuph Masauni amefanya ziara ya kikazi katika  Makao Makuu ya Uhamiaji na kutoa maagizo yafuatayo;

1. Operesheni maalum ifanywe na Uhamiaji kuyapitia makampuni yote yanoajiri wageni na kuwabaini raia wote wa kigeni wanoishi nchini kinyume na sheria ikiwemo wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania na kuziba fursa za mamia ya vijana wa kitanzania wanaohangaika kutafuta kazi, wafanya kazi tofauti na vibali vya kazi walizomba, wanaojishuhulisha na shughuli za siasa na uhalifu ikiwemo kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wananchi, kukwepa kulipa kodi na uharamia wa aina mbali mbali na kuwaondosha nchini mara moja. Tarifa ya awali ya utekelezaji wa agizo hilo iwasilishwe ofisini kwangu baada ya siku 7.
Pili. Ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili kuwabaini wahusika walotumia vibaya utaratibu wa utoaji vibali vya ukaazi vya muda (CTA), kwa kuwapatia wasiohusika, kuvitoa kiholela na kushindwa kufuatilia mpaka kupelekea kufutwa kwa vibali hivyo, na kuathiri mapato pamoja na kusababisha usumbufu kwa wageni wanaokuja nchini kwa shuhuli muhimu za muda mfupi na kuwachukulia hatua watumishi hao ambao si waaminifu ili utaratibu mpya unaoandaliwa uweze kuleta ufanisi.
Na 3. Ameagiza mchakato wa kuanzisha Mahakama ya kijeshi uharakishwe ili wezi na wala rushwa waweze kushuhulikiwa kwa haraka.

0 comments:

Chapisha Maoni