Klabu ya Real Madrid wanaongoza kwa mapato katika orodha ya vilabu 30 vya soka katika ulimwengu katika msimu wa 2014-2015 kwa mwaka wa 11 mfululizo.
Zaidi ya nusu ya klabu zenye mapato kubwa duniani zina cheza katika Ligi Kuu ya Uingereza, lakini vigogo hao wa Hispania Real Madrid na Barcelona wanaongoza kwa mapato.
Klabu ya Real Madrid walipata paundi milioni 439 katika msimu uliopita kutoka mapato ya tiketi za mechi, Haki za matangazo na vyanzo za kibiashara.
Barcelona iko kwa nafasi ya pili kwa paundi milioni 427, ikifuatiwa na Manchester United katika nafasi ya tatu katika paundi milioni 395.2.
0 comments:
Chapisha Maoni