Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameandikia Manchester United barua yenye kurasa sita kuomba nafasi ya Louis van Gaal kama meneja ya "The Red Devils",ripoti za habari zimesema.
Kulingana na jarida la The Independent, Mourinho aliandika barua hiyo jana (Jumamosi) baada ya United kushindwa 1-0 na Southampton, huku akiahidi kurejesha timu hiyo kwa hadhi yake iwapo atapewa nafasi ya kuiongoza. Kwa mujibu wa ripoti hizo, Mourinho anatarajia kutumia mtindo wake wa uongozi kukomboa Manchester United.
Mourinho alifutwa kutoka Stamford Bridge mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya mabingwa hao wa ligi ya Primea kupoteza mechi tisa kati ya 16 walizocheza.
0 comments:
Chapisha Maoni