Alhamisi, Januari 21, 2016

MARUFUKU YA NDOA CHINI YA MIAKA 18 ZIMBABWE

Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe jana (Jumatano) ilipiga marufuku kuolewa au kuozwa kwa wasichana chini ya umri wa miaka 18 katika uamuzi ambao unatarajiwa kuimarisha utetezi wa haki za watoto wadogo na kupambana na visa vya ndoa ya mapema ambavyo vimekithiri nchini humo.
Uamuzi huo uliafikiwa baada ya wanawake wawili Loveness Mudzuri mwenye umri wa miaka 20 na Ruvimbo Tsapotsi mwenye umri wa miaka 19 kufika kortini kupinga kipengee cha katiba kinachotambua miaka 16 kama umri wa kisheria ya kuolewa kwa wasichana.
Zimbabwe ni moja kati ya nchi za bara Afrika ambapo kuna visa vingi vya ndoa za utotoni. Mataifa mengine ni kama Guinea Bissau, Mauritania, Mali, Nigeria, Uganda, Burkina Faso, Ethiopia, Niger na Chad. Hii ni kwa mujibu wa kamati ya wataalamu wanaohusika na haki ya watoto katika bara la Afrika.

0 comments:

Chapisha Maoni