Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia mkazi wa Mvomero kwa tuhuma za kuwashambulia kwa kitu chenye ncha kali kichwani mkewe Elizabeth Mmari na mwanae Aisha Abeid kisha kumchoma mkewe sehemu ya juu ya ziwa la kushoto na mwanae kumchoma shingoni.
Mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji nae alikunywa maji ya betri kwa nia ya kutaka kujiua. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paul amesema tukio hilo lilitokea Januari 21 majira ya saa sita usiku kwa wahanga kusikika wakiomba msaada kwa majirani kwamba baba anatuua na baadae majirani wakaona ukimya baada ya vurugu na kukimbilia polisi.
Maji ya betri yalivyomzidi, alijaribu kutoroka na kukutwa mlangoni akiwa amelala, mtuhumiwa alikamatwa na kulazwa kwenye hospitali ya Morogoro chini ya ulinzi mkali.
Chanzo cha tukio baada ya kuulizwa, amesema mkewe na mtoto walikuwa wanaonekana kumdharau na kuamua kuchukua hatua alizochukua. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
0 comments:
Chapisha Maoni