Alhamisi, Januari 21, 2016

MAREKANI YAWEKA VIZINGITI ZAIDI VYA VIZA

Serikali ya Marekani imeanza kutekeleza sheria mpya ya viza yenye kuweka vizingiti kwa nchi ambazo raia wake kawaida hawahitajii viza kadhaa kuitembelea nchi hiyo.
Serikali ya Marekani imeanza kutekeleza sheria mpya ya viza yenye kuweka vizingiti kwa nchi ambazo raia wake kawaida hawahitajii viza kadhaa kuitembelea nchi hiyo.
Kuanzia Alkhamisi raia wa nchi 38 sasa watatakiwa kuchukua viza ya Marekani iwapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wamewahi kutembelea Iran, Syria, Sudan na Iraq. Kati ya wanaolengwa na sheria hiyo ni raia wa Uingereza, Korea Kusini, Japan, Ufaransa na Ujerumani. Aidha kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, raia wa nchi za Ulaya ambao wazazi wao ni Wairani sasa watalazimika kuchukua viza kuingia Marekani.
Mwezi uliopita Bunge la Marekani lilipitisha sheria hiyo kwa kisingizio cha kuzuia hujuma za kigaidi. Sheria hiyo ilipitishwa baada ya hujuma za kigaidi Paris Novemba 13 ambapo magaidi wa ISIS au Daesh walidai kuhusika. Hii ni katika hali ambayo, ushahidi umebaini kuwa magaidi wa ISIS walipata mafunzo kwa mara ya kwanza kabisa katika kambi za Shirika la Ujasusi la Marekani CIA nchini Jordan mwaka 2012 kwa lengo la kuiangusha sherikali ya Syria. Baadhi ya weledi wa mambo kama vile afisa wa zamani wa wizara ya fedha ya Marekani, Paul Craig Roberts, anasema Marekani ikishirkiana na NATO ilipanga hujuma za kigaidi Paris ili kutumia kisingizio cha hujuma hizo kufunga mipaka yake na kuingia vitani Syria kukabiliana na Russia ambayo imetekeleza kwa mafanikio mashambulizi ya angani dhidi ya magaidi wa ISIS tokea Septemba 30.

0 comments:

Chapisha Maoni